Katika mikakati ya kudhibiti uhalifu Kenya, Rais Uhuru Kenyatta leo amezindua mfumo mpya wa kusajili taarifa muhimu za kila mtu kuanzia wakati anapozaliwa, mfumo huo utakuwa unatunza kumbukumbu za matukio yote ya mtu kuanzia anapozaliwa ili kusaidia mambo mbalimbali ikiwemo tabia za watu kutumia vitambulisho vya watu waliofariki kupigia kura.
Usajili huo utakuwa unafanyika pale tu mtoto anapozaliwa na atapewa namba ya utambulisho ambayo atakuwa akiitumia kupata vitambulisho vyote atakavyokuwa akipatiwa.
Serikali imesema mfumo huo utasaidia katika kupambana na matukio ya uhalifu nchini humo na pia ikiwemo kuwatambua watu ambao wataingia na kutoka ndani ya nchi hiyo.
Wanatarajia zoezi la usajili wa watu wote litakuwa limekamilika ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa.
Tofauti na utaratibu uliozoeleka usajili huu utakuwa ukihifadhi taarifa za watu wote mtandaoni hivyo kutakuwa na urahisi pia wa kupatikana kwa rekodi za mtu yoyote kwa urahisi zaidi.
Hapa unaweza kuangalia habari hiyo niliyoitoa K24 TV Kenya.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook