Mahakama moja nchini Japan imemuachia huru mfungwa aitwae Iwao Hakamada aliekua akitumikia kifungo cha maisha gerezani kuanzia mwaka 1968 ambapo wanaomtetea wanasema ushahidi wa kumfunga ulitengenezwa.
Mahakama imeunga mkono kwa kusema ni kweli ushahidi wa uongo ulitengenezwa mwaka 1968 ili kumfunga kwa tuhuma za kumuua boss wake pamoja na kuiteketeza kwa moto nyumba ya boss huyo.
Hakamada alizikataa hizi tuhuma mwanzoni lakini baadae alikuja kuzikubali huku akisisitiza kuzikubali huko kutokana na shinikizo ambapo kesi yake ilirudiwa tena na kuanza kupiganiwa mwaka 1980.
Wanaomuunga mkono pamoja na jamaa na marafiki walikuwa wakiendesha kampeni za muda mrefu kuhusu bondia huyu wa zamani ambae ana umri wa miaka 78 sasa hivi na kusema damu iliyoonekana katika nguo zilizoletwa kwenye ushahidi Mahakamani ilikua ya uongo.
Vipimo vya DNA baadae vilionyesha kwamba hakukuwa na uhusiano wowote wa damu hiyo ya nguo na damu ya Hakamada mwenyewe ambapo mwaka 2007 mmoja wa Majaji watatu waliomuhukumu Hakamada kwenda gerezani mwaka 1968 K.Norimichi alisema amejutia uamuzi alioufanya.