Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuharibu miundombinu ya Reli Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini TRC Masanja Kadogosa ametoa siku 23 kwa timu ya wataalamu kuunganisha mawasiliano ya njia yaliyokatika kwa kusombwa na maji katika eneo la Mto Ugala.
Kadogosa ametembelea eneo hilo lililopo katikati ya Tabora na Katavi kuona uharibifu uliojitokeza na ametoa maelekezo “asilimia 50 ya chakula cha Kanda kinatokea huku kama hali itakuwa hivi chakula kitapanda tukachofanya ni kufanya ujenzi ndani ya maji kuunganisha tuta na treni zianze kupita”.
WAZURURAJI DSM KUKAMATWA “BAKI NYUMBANI, HATUTAKI KUTUMIA NGUVU”