Nyota wa muziki wa afrobeat wa Nigeria, Divine Ikubor, almaarufu Rema, alikutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame katika ikulu ya Kigali jana Jumapili.
Rema alihudhuria Tuzo za Muziki za Trace za 2023 mjini Kigali siku ya Jumamosi ambapo alishinda Tuzo ya Msanii Bora wa Kiafrika wa Mwaka na Wimbo Bora wa Mwaka na ‘Calm Down’.
Akizungumza wakati wa ziara yake kwa Rais, nyota huyo wa muziki alisema, “Kuja Rwanda, kunanipa vibe ya mahali naweza kupumzika na kujisikia nyumbani bila kusafiri nje ya nchi.
“A lot of time we just want to take that break, we just want to lay back… I feel like with here we can serene energy, that vibe. And I feel like it’s even going to be a bigger thing when we [Africans] start uniting.
‘muda mwingi tunatamani kupata muda wa kupumzika na inakuwa kama tunahitaji kuongeza nguvu ni msisimko…..na ninadhani itakuwa vyema sana Waafrika wakiungana’…
“Lazima niseme asante sana, Mheshimiwa Rais.”