Mwandishi maarufu wa kituo cha Televisheni kutoka Afrika Kusini amevamiwa na vibaka hadharani wakati alipokuwa akijiandaa kurusha habari Live kutoka Hospitali ya
Katika mkanda wa video umewaonyesha vijana wawili wakimvamia Vuyo Mvoko akiwa mbele ya kamera za Televisheni ya Taifa ya South Africa (SABC) ambapo alikuwa jirani na hospitali ya Milpark, Johannesburg akiripoti kuwasili kwa rais wa Zambia ambaye alikuwa akifikishwa hospitali hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Hata hivyo mwandishi huyo alisema kuwa mmoja wa wezi hao alitishia kumpiga bunduki alipokataa kumpa simu yake, hawakuonekana kutojali kamera zilizokuwa mbele yao.
Muda mfupi baadaye Mvoko ambaye ni mhariri wa kituo hicho cha habari alituma ujumbe katika ukurasa wake Twitter akisema kuwa yuko salama na kutuma video mtandaoni inayoonyesha vijana hao wakimvamia.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa wezi hao waliiba laptop na simu, Polisi wamesema maafisa wanachunguza tukio hilo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook