Mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana aliyewahi kuvichezea club mbalimbali barani Ulaya kama Rennes, Udenise na Sunderland Asamoah Gyan ameripotiwa kutokuwa vizuri kiuchumi hiyo ni kutokana na account yake kuripotiwa kuwa na salio lisilofikia Tsh milioni 2.
Asamoah ambaye aliwahi kutangazwa kama mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani katika kipindi cha mwaka 2015-2017 akiichezea club ya Shanghai SIPG ya China, kwa sasa ameripotiwa kuwa hana kitu na anapambana na hali mbaya ya kiuchumi licha ya kuvuna mamilioni akiwa China na Ulaya.
Imeripotiwa kuwa Asamoah ambaye alikuwa akilipwa mshahara wa pound 227000 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 650 kwa wiki akiichezea Shanghai SIPG, kwa sasa akaunti yake ya bank inaelezwa kuwa na pound 600 ambazo ni Tsh milioni 1.7, kwa sasa Gyan mwenye umri wa miaka 33 anacheza soka katika club ya Kayserispor ya Uturuki.
VIDEO: Furaha ya ushindi Kocha wa Simba kashangilia hadi kavua shati