Katika soka kuna mengi ya kuchekesha lakini hili la muamuzi wa Sweden linaweza likawa la kushangaza zaidi, refa mmoja raia wa Sweden amefanya maamuzi ambayo yamewashangaza wengi, kufuatia uamuzi wake wa kumuonesha kadi mbili za njano mchezaji Adam Lindin.
Refa aliamua kumuonesha kadi ya kwanza ya njano Adam Lindin baada ya kutoa hewa chafu mbele yake, baada ya mchezaji huyo kushangaa kwa kuoneshwa kadi ya njano, refa alimuonesha kadi ya pili ya njano iliyopelekea mchezaji huyo kutoka nje ya uwanja, refa alifanya maamuzi hayo akiamini tukio hilo la Adam sio la kiuchezaji.
Tukio la refa kumuonesha mchezaji kadi nyekundu kwa kutoa ushuzi uwanjani limetajwa kuwa ndio la kwanza katika, kiasi ambacho kimepelekea gumzo kubwa mitandaoni, Adam Lindin mwenye miaka 25 ni nyota wa klabu ya Pershagen SK inayoshika mkia katika Ligi Kuu Sweden.
GOAL AND HIGHLIGHTS: MO BEJAIA VS YANGA JUNE 20 2016, FULL TIME 1-0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE