Kutoka Afrika Kusini, taarifa zinaeleza kuwa ‘Nabii’ Lethebo Rabalago ambaye amekuwa akiwapulizia wafuasi wake dawa ya wadudu kwa madai ya kuwa ndio njia yake ya kuwaponya amekutwa na hatia ya shambulio.
Rabalogo amekutwa na hatia hiyo baada ya kukutwa akitumia dawa za kuuwa wadudu kuwapulizia watu huku akisema dawa hiyo itawaponya magonjwa ya saratani pamoja na Virusi va UKIMWI (VVU) mwaka 2016.
Kwenye kesi hiyo imeelezwa kuwa kitendi cha Rabalogo kupulizia watu hao dawa hizo kumewasababishia madhara makubwa ya kiafya watu watano ikiwa ni pamoja na kukohoa kwa mfululizo kwa zaidi ya miezi mitano.
LIVE: Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda amekutana na Wanasheria
https://youtu.be/TcJkqaLtF1A
Alichozungumza Kibatala baada ya Sugu kuachiwa, ametaja kilichokuwa kinakwamisha dhamana