Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Tshisekedi, amekubali kukutana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame katika juhudi za kuzima mvutano kati ya nchi hizo jirani.
Tshisekedi amekuwa kwenye rekodi akiishutumu Rwanda kwa kuunga mkono makundi yenye silaha katika eneo lenye matatizo la mashariki mwa DRC, madai ambayo Rwanda inakanusha.
Tshisekedi, ambaye alikuwa katika mji mkuu wa Angola Luanda siku ya Jumanne, aliiomba Angola kuwezesha mkutano wake na Kagame.
Rais wa DRC hakupendekeza tarehe ya mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Tete Antonio alisema Jumanne.