Forbes.com kwa mara nyingine wametaja list ya watu wenye pesa nyingi zaidi duniani ambapo wanasema kwamba hivi sasa kuna mabilionea 1,645 duniani.
Ripoti inasema kwamba wamewapata mabilionea wapya kwenye nchi kama Tanzania,Uganda,Algeria,Lithuania na nyingine.
Bill Gates ameendelea kuwa juu kwenye list akiwa na jumla ya dola za kimarekani bilioni 76 ambapo amepanda kutoka $67 bilioni za mwaka jana.
Bill Gets amekaa juu ya list hii mara 15 kwenye miaka 20 iliyopita licha ya kutumia pesa nyingi kwenye misaada.
Wamiliki wa Whatsapp Jan Koum na Brian Acton kwa mara ya kwanza wameingia kwenye list hii baada ya kuuza application yao kwa Facebook.
Mark Zuckerberg mmiliki wa Facebook ndiye billionea aliyeingiza pesa nyingi zaidi kutoka mwaka jana hadi mwaka huu. Mwaka 2013 alikuwa na utajiri wa dola bilioni 15.2 na mwaka huu ana dola bilioni 28.5 ambapo kwa mwaka mmoja ameingiza dola bilioni 13.3
Hii ndiyo list kwa wale waliopo kwenye nafasi za juu