Tia Kemp mwanamke wa zamani wa rapa Rick Ross ametoa wito kwa rapa huyo kushughulikia suala muhimu la kifedha linalohusisha elimu ya mtoto wao.
Mnamo Julai 28,2024, mpenzi huyo wa zamani wa Rozay, Tia Kemp, aliingia kwenye akaunti yake ya TikTok na kudai kuwa alihitaji kulipa kiasi kikubwa ada ya masomo ya chuo kikuu ya mwana mtoto wao mkubwa William Roberts III.
Katika klipu, wakati akionyesha bili za ada ya chuo, Tia Kemp alitoa ombi kwa Rozay na kumtaka rapper huyo atoe kinachohitajika.
“sifanya mchezo hapa, nataka umpigie babaako sasa hivi, screenshot hicho kinachoonekana hapo na umtumie….. kisha umwambie hicho ndicho ninachohitaji kwenye akaunti yangu ya benki saizi nataka umtumie sasa hivi nahitaji robo ya dola milioni 1” – ex wa Rick Ross
Hivi Karibuni Rapa Huyo alisherehekea kumaliza kumlipa Ex wake huyo pesa za zatunzo ya mtoto wao ‘William Roberts JR’, lakini cha ajabu ni kwamba anatakiwa kulipa na ada ya (Tuition) kiasi cha $200K (Tsh Milioni 540+)