Mwanamuziki wa Pop Rihanna na mkuu wa Meta Mark Zuckerberg wamewasili nchini India Ijumaa hii kwenye tafrija ya kupindukia iliyoandaliwa na tajiri mkubwa barani Asia, huku sherehe zikitarajiwa kujumuisha watu wengine mashuhuri duniani.
Watu wakubwa wanaojihusisha na teknolojia duniani, magwiji wa tasnia, mastaa wa Bollywood, wasanii wa pop na wanasiasa pia wanatarajiwa kwa sherehe za siku tatu zinazoandaliwa na bilionea Mukesh Ambani.
Sherehe ya wikendi hii ni sherehe ya kina kabla ya harusi ya mtoto mdogo Anant na mchumba Radhika Merchant, binti ya wafanyabiashara matajiri wa dawa.
Picha zilizochapishwa na vyombo vya habari vya India zilithibitisha kuwasili kwa Rihanna, Zuckerberg na mke wa mwanzilishi wa Facebook Priscilla Chan katika mji wa Ambani wa Jamnagar.
Mwimbaji wa “Umbrella” Rihanna, ambaye alijifungua mtoto wake wa pili mwezi Agosti, anatarajiwa kuongoza burudani ya Ijumaa hii katika onyesho lake la kwanza la hadhara tangu Superbowl ya mwaka jana, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.