Wiki hii ilianza na headlines za migomo.. wa kwanza ulikuwa mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar, ikafuatia stori ya mgomo wa wanafunzi wengine wa Chuo Kikuu Saint Joseph.. ikasikika nyingine ya Polisi kuuzima mgomo uliotaka kuibuka Chuo cha Ruaha Iringa.
Kabla ya hapo mgomo mkubwa kabisa uliotikisa sehemu kubwa ya TZ ulikuwa mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria ambao ulitokea mara mbili mfululizo.. leo hali haikuwa shwari Dar, kama ulitokea njia ya Buguruni kuelekea Kariakoo muda wa mchana palikuwa hapapitiki kabisa.
Mgomo huu ulihusu wafanyabiashara wenye ulemavu ambao walikuwa na vibanda vyao vya biashara eneo la soko la Karume, wanadai usiku wa kuamkia leo MAY 21 2015 Manispaa wamewavunjia vibanda vyao kinyume na makubaliano ambayo walifanya siku za nytuma kwamba watajadiliana kabla ya kuvunja.. wakaamua kufunga barabara eneo la Karume na kusababisha foleni kubwa ya magari.
Baada ya zaidi ya saa nne kupita Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi alikutana na wafanyabiashara hao wakakubaliana kukutana kesho MAY 21 2015 ili kujadili jinsi itakavyofanyika ili walipwe fidia ya hasara waliyopata na kama kutakuwa na utaratibu mwingine wa kufanya ili kuwasaidia eneo la biashara zao.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.