Kulikuwa na taarifa nyingi zilizosambazwa Mitandaoni kuhusu hali ya Kiafya ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda lakini Serikali ikakanusha kuhusu taarifa hizo na kutaarifu kuwa Waziri huyo ni mzima hajafariki, ila alikuwa India bado akiendelea kupatiwa Matibabu.
Taarifa iliyoripotiwa muda mfupi uliopita na kuthibitishwa na Serikali inahusu Msiba wa Waziri huyo, Abdallah Omar Kigoda ambaye alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.
Hiyo ni taarifa kutoka Ofisi ya Bunge ikionesha Waziri huyo amefariki leo Jioni katika Hospitali ya Appolo ambako alikuwa akitibiwa.. Serikali iko kwenye Mipango ya taratibu za kusafirisha Mwili wa Marehemu pamoja na Mazishi kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu.
“Serikali inasikitika kutangaza kifo cha Dk. Abdallah Kigoda aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kilichotokea Hospitali ya Appolo India leo.. Taarifa kuhusu kusafirisha mwili wa Marehemu na Mazishi mtaendelea kupatiwa. Dk Kigoda alilazwa tarehe 18 September 2015 ambako alikuwa akipatiwa matibabu” >>> Assah Mwambene,
Kituo cha TBC 1 wameripoti hiyo taarifa pia, unaweza kuisikiliza hapa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.