Milan na Juventus ni miongoni mwa timu zilizovutiwa na Ayyoub Bouaddi, ambaye anashika vichwa vya habari barani Ulaya kwa uchezaji wake mkali akiwa na umri wa miaka 17 pekee na alikuwa na kiwango cha ajabu dhidi ya Real Madrid.
Kulingana na Calciomercato, timu hizo mbili zenye nguvu za Serie A zinamfuatilia kiungo huyo si rahisi kuwashawishi Lille kuwaacha wachezaji wanaotaka kubaki.
Thamani yake kwa sasa ni €18M na inalazimika kukua haraka.
Milan na Juventus wote wana uhusiano mzuri na Les Dogues, jambo ambalo linaweza kusaidia iwapo wangeamua kumlenga Bouaddi.
Aidha, Rossoneri wana faida tangu Paulo Fonseca alipomfundisha msimu uliopita,bosi huyo alimfanya kuwa mchezaji mdogo zaidi kucheza kwa mara ya kwanza katika kombe la Uropa alikuwa na umri wa miaka 16 na siku 3 wakati huo.
Mkali huyo amefananishwa na Adrien Rabiot kwa sababu ya umbile lake na mtindo wa kucheza amekuwa mara kwa mara katika kampeni hii na amefikisha mechi 29 na pasi 2 za mabao akiwa na kikosi cha kwanza cha Lille hadi sasa ana mkataba hadi 2027.