Ukraine imeripotiwa kutumia kwa mara ya kwanza makombora ya masafa marefu aina ya “Storm Shadow” yaliyotengenezwa Uingereza kushambulia maeneo ya ndani ya Urusi.
Shambulio hilo limefanyika siku moja baada ya Nchi hiyo kutumia makombora ya masafa marefu ya Marekani aina ya “ATACMS” baada ya kuruhusiwa hivi karibuni na Rais Joe Biden.
Kwa mujibu wa ripoti za Vyombo vya Habari vya Uingereza, Serikali ya London hivi karibuni iliridhia matumizi ya makombora hayo ya “Storm Shadow” na tayari yameanza kutumika kuishambulia Urusi.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuongeza juhudi za kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.
Haya yanajiri wakati Rais wa Urusi, Vladimir Putin akisaini mabadiliko katika sera ya nyuklia ya Nchi hiyo miezi miwili iliyopita ambapo alisisitiza umuhimu wa kuimarisha mikakati ya nyuklia kwa usalama wa Taifa la Urusi.