Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura, Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.
Mbunge huyo aliwahi pia kufanya kazi na idhaa ya Kiswahili ya BBC, Msemaji wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe kupitia account yake ya Twitter amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.
I'm shocked. My elder Sister Hafsa Mossi Member of the @EA_Bunge has passed away, shot by criminals. R.I.P #Burundi
— Amb. Willy Nyamitwe (@willynyamitwe) July 13, 2016
ULIKOSA VITU VYA KUFAHAMU PALE SARAFU YA AFRIKA MASHARIKI ITAKAPOANZA KUTUMIKA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI