Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ametoa tathmini ya oparesheni aliyoifanya Kanda ya Ziwa ya Uvuvi Haramu miezi kadhaa iliyopita na ameagiza kuwasimamisha kazi watendaji wanaotoka kwenye Wizara hiyo.
Ameeleza kuwa viwanda 11 vilivyokuwa vinachakata minofu ya samaki ambavyo vilikaguliwa vilikutwa na makosa mengi mojawapo ikiwa ni kuchakata samaki wasioruhusiwa kuchakatwa.
“Suala la uvuvi haramu limekuwa tishio kubwa katika usalama wa raia lakini pia katika usalama wa rasilimali za taifa letu, uvuvi haramu ulikuwa unapelekea ziwa letu kwa ‘swimming pool’.” – Waziri Mpina
Aliyoyabaini Naibu Waziri wa Maji katika ziara aliyoifanya DSM
BOMOABOMOA: Nyumba zilizojengwa karibu na Reli zilivyobomolewa Arusha