Dereva Rainer Zietlof pamoja na team yake ya VW Touareg Cape to Cape Challenge wameingia nchini Tanzania kama sehemu ya ziara yao ya kuweka rekodi ya ya 3 ya kuzunguka dunia kwa kutumia gari aina ya VW Touareg.
Safari hiyo ambayo dhumuni lake kuonyesha uwezo wa aina hiyo ya gari katika mazingira yote kuanzia yale yanayokuwa na hali ya baridi kali la karibu na ncha ya kaskazini hadi joto la nyuzi joto 48 katika nchi ya Sudani.
Ziara ya Rainer Zietlof imeanzia kwenye mji uliopo North Cape nchini Norway inategemewa kumalizika Cape Agulhas nchini Afrika Kusini,timu hii itaweka rekodi ya tatu ya dunia pamoja na wenzake Matthias Prillwitz na Marius Biela.
Ziara hiyo waliianza Sept 21 ambapo wakifika Afrika kusini watakuwa wametembea nchi mbalimbali kama Norway,Finland,Sweden,Denmark,Ujerumani,Jamhuri ya Czech,Slovakia,Hungary,Serbia,Bulgaria,Turkey,Misri,Sudan,Ethiopia,Kenya na sasa Tanzania.
Wakitoka Tanzania wanategemea kuelekea Afrika Kusini wakipitia Zambia na Zimbabwe,Dereva Rainer Zietlow alianza safari zake za barabarani mwaka 2005 na kuvunja rekodi mwaka 2011-2012 kupitia safari yake iliyoitwa Panamerican kutoka Tierra del fuego hadi Alaska kwa siku 11 na saa 17.
Rekodi nyingine aliyovunja ilikua ni ile ya Russtralia ambayo ilikua kutoka Malbourne hadi St.Petersburg kwa siku 17 na masaa 11,Mradi huu wa uendeshaji wa magari upo chini kampuni ya magari ya Tehama na Volkswagen ya Ujerumani,Slovakia na Afrika Kusini.