Good news Tz zinaendelea kusikika, kila mmoja ni mtumiaji wa vyombo vya usafiri lakini baadhi ya kero ambazo tumekuwa tunakutana nazo ni kama vile foleni, uchakavu wa vyombo vyenyewe, na miundombinu duni.
Katika taarifa ya kituo cha ITV, kuna taarifa ya kuhusu kuwasili kwa mabehewa mapya 50 ya treni, akizungumza wakati wa kuwasili mabehewa hayo Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi amesema; “…Rai yangu kubwa kwa Watanzania na wafanyakazi TRL, mali hizi zinazoletwa ni za kwetu tuwe watu wa pamoja kulinda mali hizi kwa namna moja au namna nyingine. Kila Mtanzania Reli inakopita awe ni mmoja wa kushiriki katika ulinzi wa Reli hii kwa sababu tunaamini kabisa usafirishaji wa mizigo kwa njia ya Reli ambao umeanza sasa hivi unatupeleka katika matokeo makubwa ambao faida yake itapatikana kwa Tanzania wakulima kwa kusafirisha mizigo…”– Shaban Mwinjaka
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TRL amesema; “… Leo kuna hizi behewa 50 baada ya muda mfupi katika mwezi huu unaokuja wa Desemba kutakuwa na behewa 50 zingine kati ya hizo 274, mwezi huo huo Desemba kuna 50 zingine, mapema mwakani kuna behewa 174… baadaye kutakuwa na Locomotive mpya na kadhalika. Kuna miradi kama 12 ambayo TRL inatekeleza sasa hivi katika program ya BRN, hizi behewa 274 ni sehemu tu lakini kuna Locomotive mpya, mabehewa ya abiria mapya ambayo nayo mwanzoni mwa Desemba yatafika tutakutana, tutayaona…”–Mhandisi Kipalo Kisamfu
Kuisikiliza sauti ya taarifa hiyo bonyeza play hapa.