Baada ya kukamilisha msimu ambao klabu ya Real Madrid imekosa kutwaa taji lolote , uongozi wa klabu hiyo uko tayari kumfukuza kazi kocha wa timu hiyo Mtaliano Carlo Ancelotti huku orodha ya warithi ikiwa imeandaliwa .
Ripoti kadhaa nchini Hispania zimedai kuwa rais wa klabu hiyo Florentino Perez tayari amefikia uamuzi wa kumfukuza kazi kocha huyo na zimebaki saa chache kuanzia sasa ambapo mkataba wa kocha huyo na Madrid watakuwa ‘wamemalizana’.
Ancelotti mwenyewe bado hajapewa taarifa juu ya mpango wa kumfuta kazi.. Rais wa Real alikuwa na mpango huu kwa muda mrefu japo mkataba wake unaonesha imebaki mwaka mmoja kabla ya kuisha.
Ni mwaka mmoja tu umepita tangu Ancelotti alipokuwa anaonekana mfalme ndani ya Real Madrid baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa mataji mawili msimu uliopita wakati Real ilipotwaa ubingwa wa michuano ya UEFA wakiwafunga Atletico Madrid kwenye fainali pamoja na kombe la mfalme ambapo waliwafunga Barcelona.
Mapema mwanzoni mwa msimu Real Madrid walionekana kuwa tishio wakati waliposhinda mechi 22 mfululizo kwenye mashindano yote huku wakikamilisha kwa kutwaa ubingwa wa kombe la dunia kwa vilabu.
Hata hivyo mwezi January mambo yalianza kwenda kombo ambapo Real ilijikuta ikipoteza michezo mfululizo huku ikianguka kutoka kwenye kilele cha wa ligi ya Hispania kabla ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la mfalme na kukamilisha na baadae wakatolewa kwenye ligi ya mabingwa ambapo walifungwa na Juventus.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.