Usiku wa leo February 27, 2018 Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza baraza lake jipya la Mawaziri ikiwa ni baada ya kuchukua madaraka kutoka kwa Jaco Zuma.
Waziri wa zamani wa fedha Nhlanhla Nene ameteuliwa tena kushika nafasi hiyo. Nene alifukuzwa kazi December, 2015 na Rais wa zamani Jacob Zuma na nafasi yake ikachukuliwa na Des van Rooyen.
Baada ya kufukuzwa Nene Palipotokea anguko la thamani ya randi na Zuma alilazimika kumfukuza Rooyen na kumteua Pravin Gordhan, siku nne baadae ambaye pia alimfukuza kazi baadae. Katika baraza la Ramaphosa, Gordhan amerejea kama waziri wa masuala la biashara.
Pia Ramaphosa amemteua aliyekuwa mpinzani wake katika kuwania uongozi wa Chama cha ANC, Nkosazana Dlamini-Zuma kuwa waziri kwenye ofisi ya rais.
Ramaphosa alimshinda Zuma kwenye Uchaguzi wa ANC na kuchaguliwa kushika wadhifa wa Uenyekiti wa chama hicho.
KIGWANGALLA ATOA MIEZI 9 “KWA SASA HATUTOTUMIA NGUVU KWANZA” , BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA