Beki wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na club ya Real Madrid ya Hispania Roberto Carlos amefunguka kuwa kocha wake wa zamani akiwa Inter Milan Roy Hogson hajui mpira.
Roberto ,46, ameeleza hayo akisema kuwa Hogson hajui mpira kwa sababu alikuwa analazimisha beki wa kushoto (yeye) akacheze katika eneo la kiungo.
“Roy Hogson aliniharibu alinitaka nicheze katikati ya viungo, nisingepata nafasi ya kwenda kucheza Copa America katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil 1997 ni kwamba hajui sana kuhusu mpira wa miguu”>>> Roberto Carlos
Roberto Carlos alicheza msimu mmoja Inter Milan 1995/96 na kuamua kuondoka na kwenda Real Madrid ambako alishinda mataji 13, Carlos aliondoka akiamini kuendelea kukaa chini Hogson na mifumo yake angepoteza nafasi Brazil.