Wakati Bastian Schweinsteiger, Matteo Darmian na Morgan Schneiderlin wakielekea Old Trafford kukamilisha ndoto zao za kujiunga na moja ya vilabu vikibwa duniani, Robin van Persie yeye ameondoka kwenye klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa kiholanzi ambaye alijiunga na Manchester United mnamo mwaka 2012 akitokea Arsenal kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 24, sasa anaelekea klabu ya Fernabahce.
Mshambuliaji huyo jana alisafiri kwenda Istanbul na alipokelewa kama mfalme na mashabiki wa klabu yake mpya.
Van Persie ambaye aliiwezesha United kushinda ubingwa wa 20, akifunga magoli zaidi ya 20, msimu uliopita alikumbwa na balaa la majeruhi akiishia kufunga magoli 10 tu.
“Nimekuja kujiunga na klabu nzuri na kubwa, ni heshima kubwa kwangu.” Alisema Van Persie.
Fenerbahce walithibitisha Alhamisi kwamba wameingia kwenye mazungumzo na United juu ya uhamisho wa ndachi huyo.
Van Persie sasa anaungana na mchezaji mwenzie wa zamani wa United, Luis Nani.