Mapema mwezi huu, mshambuliaji wa Real Madrid Rodrygo alimtaja mshambuliaji wa Al-Nassr Cristiano Ronaldo kuwa kielelezo chake anachokitazama.
“Cristiano Ronaldo ni role model wangu. Ni kama shujaa. Nimekuwa nikimfuata tangu nikiwa mdogo. Ni mchezaji niliyemkubali sana binafsi simfahamu sana lakini nilimuona mara moja na nilikuwa niliweza kupiga picha naye ilikuwa ni moja ya wakati maalum kwani nilipata fursa ya kukutana na mfano wangu wa kuigwa.”
Akisifu maisha marefu ya fowadi huyo wa zamani wa Real Madrid, Rodrygo alihitimisha:
“Hata akiwa na umri wa miaka 39, anaendelea kucheza na kufunga mabao mengi, hivyo bila shaka ni chanzo kikubwa cha msukumo kwangu.”
Ronaldo, ambaye alifikisha umri wa miaka 39 mapema mwezi Februari, hajaonyesha dalili zozote za kuacha kazi yake ya kulipwa. Amefunga mabao 34 na kuandikisha asisti 11 katika mechi 35 za Al-Nassr kufikia sasa msimu huu.
Wakati akiwa Real Madrid, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye mechi 205 alishinda mataji 16, yakiwemo mataji manne ya UEFA Champions League na mawili ya La Liga,aifunga mabao 450 katika rekodi ya klabu katika mechi 438 pekee, na kusajili asisti 131 katika mchakato huo.