Beki wa klabu ya Manchester United Marcos Rojo ameingia kwenye headlines baada ya kuweka picha katika mitandao ya kijamii zikimuonesha akifanya shughuli za nyumbani kama kuosha vyombo na kadhalika. Marcos Rojo sio mahiri tu uwanjani kumbe hata kwenye kazi za nyumbani huwa hamuachii mkewe pekee.
Marcos Rojo alipost picha nyingine ikimuonesha yeye pamoja na mkewe Eugenia Lusardo wakiwa kitandani wakipata kifungua kinywa, inadaiwa kuwa Marcos Rojo alimuandalia kifungua kinywa mkewe Eugenia Lusardo wakiwa kitandani.
Hata hivyo beki huyo ameutumia muda huu wa mapumziko ya mechi za kimataifa kukaa na kufurahia na mkewe kwani hajaitwa katika kikosi cha Argentina kinachojiandaa kucheza na Ecuador na Paraguay kutokana na kutopona kwa tatizo lake la hamstring katika mguu wake wa kulia.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE