Sikuwa nafahamu, leo nimejua kwamba kumbe kampuni inayotengeneza magari ya Rolls Royce ina miaka 111 tangu imeanzishwa!
Ni kampuni chache zilizoweza kudumu kwa kipindi kirefu kama hicho na bado zikawa na nguvu kubwa ya uzalishaji na kutawala sokoni pia.
Kampuni hii ilianza rasmi mwaka 1904, Uingereza baadaye wakaanzisha uzalishaji wa magari hayo Marekani.
Rekodi ya mauzo ya magari hayo mwaka 2014 imekuwa ya pekee, wameuza magari 4,063 huku uuzwaji wa magari hayo ukitegemea soko kubwa la Abu Dhabi, UK, Marekani na China.
Gari hizi tumeziona sana katika video za muziki hasa za wasanii wa Marekani, unaambiwa hizi ni moja ya gari zilizokaa kistarehe na za bei juu zaidi duniani kwa sasa.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook