Mtaalamu wa uhamisho wa kandanda Fabrizio Romano amefichua kuwa Los Angeles FC wamefikia makubaliano ya mdomo kumsajili mshambuliaji wa AC Milan Olivier Giroud.
Romano alifichua haya katika tweet kupitia akaunti yake ya X siku ya Jumatano.
Alitweet,
“LAFC wamefikia makubaliano ya mdomo ya kumsaini Olivier Giroud kwa kandarasi itakayotumika hadi Desemba 2025!
“Baada ya nia kufichuliwa mnamo Oktoba na zabuni rasmi mapema wiki hii, kuna makubaliano ya awali.
“Hakuna kilichosainiwa bado lakini karibu na kufanywa. Haya twende, hivi karibuni.”
Giroud, 37, alijiunga na Milan mwaka 2021 akitokea Chelsea.