Mahojiano ya Cristiano Ronaldo na mwanahabari Piers inawezekana yakawa yanathibitisha kuwa huenda baada ya Kombe la Dunia 2022 Ronaldo akaondoka Man United kutokana na mahusiano na Kocha Erik Ten Hagen kuvurugika.
Ronaldo alirejea Man United 2021 akitokea Juventus ikiwa ni miaka 12 tangu aondoke Man United 2009 na kujiunga na Real Madrid ya Hispania ila baada ya kumalizana na Juventus alihusishwa kujiunga na Man City kabla ya baadae kubadili maamuzi.
Ronaldo akiri ni kweli alitaka kujiunga na Man City ila Kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson alimzuia na kumwambia huwezi kwenda kwa mahasimu.
“Nilifuata moyo wangu kwa kugusa kifua changu, (Ferguson) aliniambia ni haiwezekani kwa wewe (Ronaldo) kwenda Man City, nikasema sawa boss”>>> Ronaldo