September 10 mwaka huu alinukuliwa Rais wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Florentino Perez kuhusiana na stori za klabu ya PSG ya Ufaransa kuhitaji kumsajili Cristiano Ronaldo akitokea Real Madrid. Rais wa Real Madrid alidaiwa kukataa kabla ya siku hiyo kukubali kuwa Ronaldo anaweza kuuzwa ila kwa dau la pound milioni 728.
Stori kutoka klabu ya Orlando City ya Marekani inahitaji kumsajili Cristiano Ronaldo kutokea Real Madrid, lakini haijulikani wanahitaji kumsajili kwa kiasi gani. Mmiliki wa klabu ya Orlando City Flavio Augusto Da Silva amethibitisha kumuhitaji Cristiano Ronaldo katika timu yao. Flavio Augusto Da Silva amekiri kuwa Ronaldo ni bora kuliko Lionel Messi na wanafikiria kumsajili nyota huyo.
“Kiukweli tunampenda Ronaldo sana tusingeweza kutaka kumsajili bila ya kufikiria, Ronaldo amekamilika kuliko Lionel Messi anaweza kufanya vizuri MLS kuliko Messi, tunamatumaini tutamsajili msimu huu unaofuata tulisikia kuwa alikuwa anapenda kuja kucheza Ligi Kuu Marekani”>>> Flavio Augusto Da Silva
Orlando City ni moja kati ya klabu inayoshiriki Ligi Kuu Marekani yenye makao makuu yake Florida, kwa sasa timu ya Orlando City ina mchezaji bora wa Dunia wa mwaka 2007 Ricardo Kaka. Orlando City inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani ambayo inachezwa kwa kikanda ipo nafasi ya saba katika timu 10 zinazoshiriki Ligi hiyo ukanda wa mashariki.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE