Licha ya kuwa mwaka 2015 staa wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kufanya mipango yake mingi na kwa asilimia kubwa kufanikiwa, miongoni mwa ishu alizofanya Cristiano Ronaldo kwa mwaka 2015 ni kuzindua movie ya maisha yake halisi, perfume, viatu vyake lakini hii sio taarifa njema kwake.
November 27 kutoka El Economista wametangaza kuwa kampuni ya vifaa vya michezo ya kimarekani Nike imetangaza kumtaja staa wa FC Barcelona Neymar kuwa ndio staa namba moja kwa sasa anayeuza brand ya bidhaa zao, rekodi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Ronaldo kwa miaka kadhaa ila November 27 Neymar ndio ameandikwa kumzidi Ronaldo.
Stori kutoka 101greatgoals.com inatajwa kuwa Neymar kwa mwaka 2016 ndio anatazamiwa kuwa staa atakayefanya vizuri kwa mauzo ya Nike na ndio maana kwa sasa anatajwa kuwa namba moja na Ronaldo kushuka, licha ya kuwa Ronaldo amefanya vizuri kwa miaka kadhaa. Ronaldo na Neymar wote wanamkataba wa kutangaza bidhaa za Nike .
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.