Chama cha Rotary Club pamoja na wadhamini mbalimbali kama Watercom,Asas,Azam na Airtel leo wamekutana na Chama cha maalbino Tanzania kwenye hospitali ya Ocean Road jijini Dar ea salaam kwa lengo la kuwapa vifaa ambavyo kwao ni changamoto kubwa kwenye ngozi zao.
Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa chama cha watu wenye ualbino Tanzania Godson Mollel amesema,changamoto kubwa wanazo zipata ni upatikanaji wa lotion,nguo za mikono mirefu pamoja na kofia kwani yakifanyika hayo watakuwa wametibu swala la saratani ya ngozi.Pia ametoa wito kwa serikali kuwa wanahitaji marekebisho ya sera yafanywe mara kwa mara kwani nao wanahitaji kwenda na mfumo.
Kwa upande wake Rais wa Rotary club,Nazeer Tajudeen amesema kuwa kipaumbele chao kikubwa ni kuhakikisha watu wenye ugonjwa wa saratani ya ngozi(Albino)wanapata mahitaji yao bila kukosa mahitaji kwani watu wenye ualbino wanahitaji mahitaji yote kama wengine wapatavyo.
Nae mwakilishi kutoka chama cha ualbino ,Swaumu Waziri amewashukuru sana Rotary Club pamoja na wadhamini wote kwa kuonyesha kuwajali na kuwathamini sana watu wenye ualbino na pia wito wake kwa serikali ni waendele kuwakumbuka wenye saratani ya ngozi kwenye nafasi za ajira na misaada mbalimbali.