Serikali Mkoani Geita imesema itaendelea kushirikiana na Shule Binafsi katika kusaidia kuinua Ufaulu wa Wanafunzi katika shule mbalimbali zikiwemo shule za Mashirika ya Dini na Shule Binafsi huku walimu wakipongezwa kwa Jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kulea watoto katika Misingi ya Kiroho.
Hayo yameelezwa na Afisa Elimu Mkoa wa Geita, Anthony Mtweve wakati wa Mahafari kwanza ya Kidato cha nne yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Royal Family Mjini Geita huku akiimiza wazazi kuwapokea wanafunzi hao ambao wamehitimu hivi Karibuni.
“Pongezi zangu zaidi na zaidi ni kwa wazazi niwapongeze tena wazazi kwa namna ambavyo muliona kwamba Royal Family ilisitaili kupeleka watoto kama mulivyosema shule hii ni Mahafari ya kwanza na wazazi tumepeleka watoto hawa mkiwa hamna wasiwasi kwa kweli ni Moyo wa Ujasili, ” Afisa Elimu Mkoa wa Geita, Mtweve.
Nami Mlwafu ni Meneja wa Taasisi za Royal Family amesema wamekuwa wakitumia Njia mbalimbali za Kuelimisha wanafunzi kupitia masomo wanayofundishwa shuleni hasa kichocheo kikubwa kikiwa ni kumbadilisha mwanafunzi kuwa na tabia nzuri na yenye kupenda kusoma akiwa nyumbani na Shuleni.
“Vijana wetu wengi kama ulivyoona siku ya leo wako vizuri kwenye Maadili na wanakuwa hivyo tunashirikiana pia na wazazi kuwa na wazazi karibu kuhakikisha kwamba mtoto kutokea nyumbani na hata tunapokuwa naye hapa tunakuwa tayari kumsaidia kimaadili watoto wetu kusema kweli ni kielelezo kama Kauri mbiu yetu inavyosema, ” Meneja Taasisi za Royal Family.
Baadhi ya Wazazi waliohudhuria katika Mahafari hayo wamesema Msingi Mkubwa katika kulea watoto ni kuwalea katika Misingi ya kiroho kwani Maadili yamekuwa ni kikwazo kwa Jamii hasa linapokuja suala la kuharibiwa na kupitia Masuala mbalimbali huku akiwashukuru walimu kwa ushirikiano Mzuri katika kutoa elimu .
Aidha wameushukuru Uongozi wa Shule ya Sekondari Royal Family kwa malezi mazuri kwa kipindi chote cha Masomo kutoka kwa watoto wao huku wakihimiza Serikali kufundisha Masomo ya Kiroho kwani ni kichocheo kikubwa kwa mwanafunzi kufanya vizuri.