Jumapili ya Pasaka April 1, 2018 Padri wa kanisa moja la Katoliki nchini Congo alitekwa na wanaume ambao walikuwa na silaha ambao waliomba kupewa Dola za Marekani 500,000 sawa na Shilingi bilioni 1.2 ili wamwachie huru.
Jana April 6, 2018 watekeaji hao walimwachia huru Pardi huyo Celestin Ngango baada ya kupewa pesa hizo, lakini inaripotiwa kuwa watu wengine watatu waliokuwa pia wametekwa kuwa wameuawa.
Kwa mujibu wa Kituo cha Utafiti cha Kukuza Amani, Demokrasia na Haki za Binadamu CEPADHO Padri Ngango ni mmoja kati ya watu 10 ambao waliotekwa nyara katika wilaya ya Rutshuru.
Tsunami kubwa kuwahi kutokea duniani