Alhamisi ya September 7 2017 Rais wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amekabidhiwa ripoti ya uchunguzi ya madini ya Tanzanite na Almasi uliyofanywa na kamati mbili maalum zilizokuwa zimeundwa na spika wa Bunge Job Ndugai.
Ripoti ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi ambayo imekabidhiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa Rais Magufuli, imemtaja waziri wa TAMISEMI George Simbachawene, hivyo muda mchache baada ya kutajwa amefanya maamuzi.
Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ameripotiwa kuandika barua ya kujiuzulu baada ya jina lake kutajwa katika uchunguzi huo, uchunguzi huo ulifanywa na kamati mbili zilioundwa na Spika wa Bunge Job Ndugai.
VIDEO: Rungwe afunguka baada ya kuachiwa kwa dhamana