Timu ya taifa ya Uganda maarufu kama The Cranes tayari imetangaza kikosi chake kitakachopambana na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars katika mchezo wa mwisho wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika AFCON 2019 nchini Misri.
Kwa upande wa Uganda wao wamefanikiwa mapema kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika 2019 kutokana kuwa na point 13 ambazo hakuna timu ambayo inazo katika Kundi lao lilopo na timu za Tanzania, Uganda wenyewe, Cape Verde na Lesotho.
Kocha mkuu wa Uganda Sebastien Desabre ametangaza kuita wachezaji 15 wanaocheza nje ya Uganda na majina 31 ambayo yatachujwa hadi kufikia 9 na kuungana na 15 katika mchujo wa mwisho katika mchezo dhidi ya Tanzania March 24 2019 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Jumla ya wachezaji 24 wa Uganda watakwenda kuweka kambi nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa mwisho dhidi ya Tanzania ambao ni muhimu kwao na wanahitaji ushindi, Tanzania wapo nafasi ya pili ila Kundi hilo timu zote tatu zilizosalia ukichana na Uganda zote zina nafasi ya kufuzu kama zitapata matokeo mazuri katika mchezo wake wa mwisho.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake