Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wamezindua chapa mpya kwa bidhaa yao ya OTT (Application), itakayokuwa ikijulikana kwa jina la StarTimes ON. Bidhaa hiyo inakuwa ya kwanza kabisa barani Africa kutoa huduma ya maudhui mtandaoni kwa teknolojia ya kisasa zaidi ili kuongeza burudani na utazamaji mzuri zaidi.
Uzinduzi huo wa StarTimes ON umekuja baada ya App ya awali (StarTimes App) kufanyiwa maboresho makubwa na kuwa StarTimes ON. StarTimes ON imekuja na Luninga Mubashara, VOD pamoja na video fupi ambazo zitakuwa na maudhui mbali mbali kuanzia Habari, michezo, tamthiliya, muziki, burudani, makala, vipindi vya watoto pamoja vipindi vya dini.
“Tutaongeza chaneli nyingi zaidi za Kimataifa ili kuongeza Burudani, lakini kwa sasa zipo chaneli kama Fox News, BBC World News, France 24, AMC Movies, Fox Life na bila kusahau filamu nyingi za Kibongo msimu huu wa Siku Kuu ambazo zitakujia kupitia ST Swahili”. Aliongeza
Wakati huo huo, StarTimes ON inathamini chaneli na maudhui ya ndani ndio maana imeongezewa chaneli mbali mbai za kiafrika kama vile TBC 1, NTA, ZNBC, TVM, KTN, RTI na RTs ambazo zinapatikana katika nchi husika.
Pamoja na hayo yote, kupitia StarTimes ON watumiaji wanaweza kuwapigia kura washiriki wawapendao katika shindano la Bongo Star Search, wanaweza kutazama Show mbali mbali za washiriki wa BSS na kuwatumia maua majaji wa BSS, StarTimes ON ni App ya kwanza Tanzania yenye aina hiii ya utumiaji.
Kupitia StarTimes ON watumiaji wanaweza kutazama michezo mbalimbali kama vile Ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga, Ligi ya Ufaransa (Ligue 1), ligi ya UEFA EUROPA inayoendelea Alhamisi wiki hii. Kwa sasa Mechi za Bundesliga na Ligue 1 zinaonekana moja kwa moja pia kutazama marudio ya mechi hizo muda wowote na sehemu yoyote.
EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?