Rubani mmoja amefariki baada ya helikopta kuanguka kwenye paa la hoteli moja katika mji wa Cairns kaskazini mwa Queensland.
Ndege hiyo ilianguka kwenye hoteli ya DoubleTree majira ya 01:50 usiku kwa saa za eneo hilo siku ya Jumatatu, na kuwaka moto ambapo mamia ya wageni walihamishwa eneo salama.
Mamlaka inasema mtu pekee aliyekuwa kwenye helikopta hiyo ndiye aliyefariki katika eneo la tukio, huku wageni wawili wa hoteli hiyo – mwanamume mwenye umri wa miaka 80 na mwanamke mwenye umri wa miaka 70 – walipelekwa hospitalini na wako katika hali nzuri.
Polisi wa Queensland na waangalizi wa usalama wa anga wanachunguza mazingira ya ajali hiyo, huku kampuni inayokodisha helikopta hiyo ikisema ilikuwa katika safari ambayo “haikuidhinishwa”.
Amanda Kay, ambaye alikuwa akiishi katika hoteli kwenye eneo kuu la esplanade huko Cairns, alielezea kuona helikopta ikiwa eneo la “chini zaidi”, bila taa katika hali ya hewa ya mvua.
Kulingana na ripoti katika news.com.au.Helikopta iliyoanguka kwenye paa la hoteli katika mji wa kaskazini mwa Queensland wa Cairns nchini Australia siku ya Jumatatu (Ago 12), na kumuua rubani, huenda iliibwa katika uwanja wa ndege wa Cairns Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo ya ndege Aaron Finn alisema .
“Tunapoendelea kuunga mkono kikamilifu uchunguzi unaoendelea, hatutatoa maoni zaidi kwa sasa.”
Utambulisho wa rubani bado haujajulikana katika hatua hii. Nautilus Aviation imethibitisha kuwa wafanyakazi wake wote walikuwa tayari wamehesabiwa siku hiyo na wamepewa siku ya mapumziko kufuatia tukio hilo.
Kwa mujibu wa habari, moto ulizuka mara baada ya helikopta hiyo kuanguka. Wahudumu wa afya walifika eneo la tukio baada ya saa 2 asubuhi na kumpima mgonjwa wa kiume aliyekuwa na majeraha ya kutishia maisha.
Mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 80 na mwanamke mwenye umri wa miaka 70 walitibiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Cairns.