Rubani Samwel Balina Gibuyi wa ndege ya Shirika la PAMS Foundation amepotea toka aruke na ndege hiyo October 18, 2021 saa 9 na hadi leo hajapatikani wala ndege hiyo haijaonekana ambapo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro ameiambia AyoTV kwamba Ndege hiyo ilikua inakwenda Hifadhi ya Selous Kanda ya Kingupila na ilitarajiwa ikiondoka Tunduru itapita maeneo ya anga ya Kijiji cha Kajima, Hifadhi ya Selous, Liwale, halafu ingerudi tena Selous.
“Wenzetu wa PAMS walipoitafuta kupitia kifaa maalumu (tracker) hawakuiona na hapohapo juhudi za kuitafuta zikaanza na baadae Mamalaka za Anga Tanzania ziliongeza nguvu tulipata ndege nne na tukapata Helikopta moja na zikaanza kuitafuta, zilipita kwenye njia yote ambazo ndege hiyo ilitarajiwa kupita na kwenye mito yote mikubwa lakini doria hizi za anga hazikufua dafu”
“Hata tarehe 20 pia hazikua dafu, tukatengeneza Timu za utafutaji za ardhini lakini mpaka sasa bado, tunaitafuta hii ndege sababu ya Rubani aliekuwa anaiendesha na ndege haikua na Mtu mwingine” ——Mkuu wa Wilaya ya Tunduru