Rudolf Erasmus alikuwa akisafirisha watu wanne katika ndege ndogo alipogundua kitu baridi kilikuwa kikimpapasa kwenye ngozi yake juu ya shati lake hapo awali, alidhani chupa yake ya maji ilikuwa ikivuja ndipo alipogeuka akagundua ni nyoka huyo akiteleza kwenye mwili wake.
Alisema alitambua kuwa nyoka huyo alikuwa nyoka aina ya Cape cobra ambaye angeweza kuua watu tisa kwa kuwauma mara moja.
“Nilihisi hali hii ya ubaridi kikitembea juu ya shati langu nilipogeuka upande wa kushoto na kutazama chini, nilimwona cobra… akirudisha kichwa chake nyuma chini ya kiti.”
Erasmus alijaribu kumshika nyoka huyo na kufanikiwa kumdhibiti kwa kutowaambia abiria kuwa mnyama huyo alikuwa ndani ya ndege hiyo.
Hata hivyo, ilimbidi kuwaambia baadae kwamba cobra ilikuwa chini ya kiti chake, na cha kushangaza, abiria walikuwa watulivu sana kuhusu hali hiyo.
Baada ya ndege kutua, alivuta kiti chake mbele, na cobra alikuwa imejikunja chini yake, lakini alitoweka muda mfupi baada ya wachunguzi kuikagua ndege hiyo.