Russia imezidisha mashambuli ya makambora dhidi ya mji wa Ukraine wa Bakhmut ikitumai kuuteka mji huo ifikapo Jumanne, afisa wa cheo cha jenerali katika jeshi la Ukraine anayehusika na ulinzi wa mji huo uliozingirwa alisema Jumapili, akiahidi kufanya kila liwezekanalo kuzuia jambo hilo lisitokee.
Jenerali Oleksandr Syrskyi, kamanda wa vikosi vya ardhini vya Ukraine, amesema kwamba wanajeshi wa Russia wamezidisha mashambulizi ya makombora kwa kutumia silaha nzito dhidi ya mji huo, na wameanza kutumia vifaa vya kisasa na kupanga upya wanajeshi.
Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha ripoti hizo.
Wizara ya Mambo ya nje ya Saudi Arabia katika taarifa yake imesema, baada ya kuanza kwa mazungumzo ya awali, Jumamosi iliyopita, mazungumzo hayo yataendelea katika siku zijazo kwa lengo la kumaliza vita ambavyo vimeendelea kwa wiki ya tatu sasa.
Aidha, Mawaziri kutoka nchi za Kiarabu waliokutana jijini Cairo, wamekubaliana kuendelea kufuatilia kwa karibu kinachoendelea nchini Sudan kwa lengo la kupata suluhu ya kusitisha mapigano yanayoendelea ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia.
“Leo, ni muhimu sana kuchukua maamuzi haraka iwezekanavyo ili kuzuia vitendo vya adui,” Syrskyi alisema kwenye mtandao wake wa Telegram baada ya kile alichosema ilikuwa kuwajulia hali wanajeshi ambao wako kwenye mapambano katika mji wa Bakhmut.
“Russia bado wanatumai kuuteka mji huo ifikapo tarehe 9 Mei. Wajibu wetu ni kuzuia hilo lisitokee.”
Tarehe 9 Mei ni maadhimisho ya siku ya ushindi nchini Russia ikiwa kumbukumbu ya ushindi dhidi ya utawala wa Wanazi wa Ujerumani.