Rais wa Kenya William Ruto amewataja viongozi wa upinzani na kuwarejesha kazini mawaziri wengine waliofutwa kazi katika baraza jipya la mawaziri kufuatia maandamano ya kuipinga serikali yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 50.
Rais alimtaja kiongozi wa wachache Opiyo Wandayi kuwa waziri wa nishati na mbunge John Mbadi kama waziri wa fedha, ambao wote ni wa chama cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga.
Ruto Jumatano alitaja kundi la pili la mawaziri 10 lililojumuisha mawaziri wanne na mwanasheria mkuu aliyemfuta kazi takriban wiki mbili zilizopita.
Alikuwa ametaja kundi la kwanza la mawaziri 11 wiki iliyopita.
Wateule wa baraza la mawaziri wanapaswa kuidhinishwa na wabunge katika Bunge la Kitaifa kabla ya kuteuliwa.
1. Hazina – John Mbadi
2. Biashara – Salim Mvurya
3. Utalii – Rebecca Miano
4. Nishati – Opiyo Wandayi
5. Madini – Hassan Joho
6. Michezo – Kipchumba Murkomen
7. Kazi – Alfred Mutua
8. Vyama vya Ushirika – Wycliffe Oparanya
9. Utumishi wa Umma – Justin Muturi
10. Jinsia – Stella Langat