Serikali ya Rwanda kupitia kwa Waziri wake wa elimu Valentine Uwamariya imesema shule zote zitafunguliwa ifikapo mwezi Novemba mwaka huu kwa kuanza na kufungua vyuo vikuu.
‘’Shule zitafungua kwa awamu tofauti kuanzia ngazi ya Vyuo Vikuu ambavyo tunatarajia vitafungua milango mwezi ujao, shule nyingine kama sekondari, shule za msingi na chekechea tunatarajia kwamba zitakuwa zimeshafunguliwa’’ Uwamaria
Wizara ya Elimu imesema shule zitatakiwa kuzingatia masharti yaliyopo ya kujilinda na Covid -19 kama kuwa na sehemu ya kuosha mikono, kuvaa barakoa kwa kila mwanafunzi na kuacha nafasi ya mita moja kati ya wanafunzi.
Machi 15 mwaka huu Serikali ya Rwanda ilitangaza kuchukua hatua kadhaa za dharura kukabiliana na janga la virusi vya Corona ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa shule zote za umma na za kibinafsi, maeneo ya kuabudu na sehemu zote za umma, kama sehemu ya juhudi za kukabiliana na virusi vya corona.
TAZAMA VIJANA 997 WAKIHITIMU MAFUNZO YA AWALI YA KIJESHI