Idara ya Upelelezi ya Rwanda (RIB) na Wizara ya Mazingira ya nchi hiyo wamezindua matumizi ya ndege zisizo na rubani (droni) kupambana na uhalifu wa mazingira.
Uhalifu wa mazingira ni moja ya changamoto nne kubwa za uhalifu duniani, na uhalifu huo unaongezeka kwa asilimia tano hadi saba kila mwaka. Droni zitakusanya taarifa, kufanya ukaguzi kwa ajili ya kuzuia na kusaidia uchunguzi wa uhalifu wa kimazingira.
Waziri wa Mazingira wa Rwanda Jean d’Arc Mujawamariya amesema ndege hizo zitasaidia kukabiliana na kudhibiti shughuli zinazoharibu mazingira, ikiwa ni pamoja na uharibifu wa ardhi, uchafuzi wa maji, na ukataji miti katika maeneo yaliyohifadhiwa.
Ndege zisizo na rubani zitakusanya taarifa, kufanya ukaguzi kwa ajili ya kuzuia, na kusaidia uchunguzi wa uhalifu wa kimazingira.
“Ndege hizo zitasaidia kukabiliana na kudhibiti shughuli zinazoharibu mazingira yetu ikiwa ni pamoja na uharibifu wa ardhi, uchafuzi wa maji, na ukataji miti ovyo katika maeneo yaliyohifadhiwa,” alisema Waziri wa Mazingira Jeanne d’Arc Mujawamariya.
“Tunaishukuru Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda (RIB) iliyoungana nasi katika mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira ambapo ilifanya kampeni za uhamasishaji kuhusu uhalifu wa mazingira, kubaini wahanga wa uhalifu huo wa mazingira, wakosaji na kufungua majalada ya kesi kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka,” alisema.