Raia wa Rwanda wanatazamiwa kupiga kura Julai 15, 2024, kuwachagua manaibu wao na rais, huku mkuu wa sasa wa nchi Paul Kagame akiwania muhula wa nne, Tume ya Uchaguzi ilitangaza Jumanne.
Paul Kagame, 66, amekuwa kiongozi mkuu wa nchi hii ya Maziwa Makuu tangu mwisho wa mauaji ya kimbari ya 1994. Alirejeshwa mamlakani kwa zaidi ya 90% ya kura katika chaguzi za 2003, 2010 na 2017.
“Nchini kote, tarehe ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri na manaibu 53 kutoka kwenye orodha iliyopendekezwa na mashirika ya kisiasa au kwa wagombea binafsi ni Julai 15, 2024,” Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye X (ex-Twitter) ilisema.
Wagombea wataweza kufanya kampeni kuanzia Juni 22 hadi Julai 12, iliongeza.
Wabunge 24 wanawake, wawakilishi wawili wa vijana, na mwakilishi mmoja wa Wanyarwanda wenye ulemavu pia watachaguliwa na vyuo na kamati za uchaguzi mnamo Julai 16, Tume ilisema.
Mnamo Machi, serikali ilitangaza kuwa uchaguzi wa rais na wabunge utafanyika siku hiyo hiyo.