Wizara ya Afya nchini Rwanda jumatatu imezindua kampeni ya nchi nzima ya kutoa dozi ya pili ya chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka saba.
Kwa mujibu wa mkuu wa Kitengo cha Chanjo katika Kituo cha Matibabu kwa Kutumia Dawa nchini humo, Hassan Sibomana, zoezi hilo litaendelea mpaka ijumaa wiki hii, likiwalenga watoto wote walio ndani ya umri huo.
Amesema awamu ya kwanza ya chanjo hiyo iliyotolewa Julai ilifanikiwa sana, huku watoto milioni 2.9 wakipata chanjo hiyo, na kuongeza kuwa wanategemea watoto hao watapata dozi ya pili.
Kampeni hii nchini Rwanda imezinduliwa baada ya ripoti za mlipuko wa ugonjwa wa Polio katika nchi jirani na Rwanda.
Kesi ya mwisho ya Polio nchini humo ilirekodiwa miongo mitatu iliyopita.
Tazama pia…..