Njia za usafirishaji hutofautiana kwenye nchi na nchi kutokana na maendeleo yake ya teknolojia na miundombinu. Kwenye pitapita za mitandaoni millardayo.com imekutana na aina ya usafiri unaotumika katika Kisiwa cha Madagascar kilicho kwenye Bahari ya Hindi.
Katika kisiwa hiki moja kati ya usafiri mkuu ni gari aina ya Citroen’s 2CV ambazo hutumika kama taxi. Citroen’s 2CV inaelezwa kuwa ni gari ambayo kiasili ilikuwa na bado inatumiwa katika maeneo ya kijiji nchini Ufaransa, na pindi wakoloni wa Kifaransa walivyoondoka kisiwani hapo baada ya ukoloni, magari haya yaliendelea kutumika.
Ni magari ya model ya zamani sana lakini bado ni usafiri maarufu sana Madagascar kwani unaelezwa kuwa ni magari magumu ambayo hayahitaji gharama nyingi za mafuta na matengenezo na pia hudumu kwa miaka mingi sana.