Baada ya kinyang’anyiro cha uchaguzi wa udiwani nchi nzima kumalizika jana November 26, 2017 na chama cha ACT wazalendo kushindwa kupata hata kata moja ya ushindi, kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe ameongelea suala hilo.
Zitto amesema kuwa wao kama chama wamekubali matokea hayo na kwamba wapiga kura wameamua na wao wamekubaliana na hilo na kwa sasa wanafanya tathmini ya matokeo ya nchi nzima na baadaye watazungumza na wananchi.
Ameeleza pia kuwa uchaguzi huu ulikuwa fursa ya kuzungumza na wananchi na kufikisha ujumbe wao kwani kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara kunawanyima fursa ya kufanya hivyo.
“Tutazienzi kwani ndio haki yetu. Tunajiandaa na chaguzi ndogo zinazokuja ikiwemo za Ubunge kwenye majimbo yaliyowazi. Tutatumia mafunzo tuliyoyapata kwenye chaguzi ndogo hizi kujipanga na chaguzi zinazokuja.” – Zitto Kabwe
Ulipitwa na hii? “Ambae safari imemshinda ashuke mwenyewe”- ZITTO KABWE