Utafiti mpya uliofanyika na kuchapishwa kwenye vyombo vya habari mbalimbali duniani unaeleza kuwa ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu yaani dementia huweza kupungua hatari yake kwa watu walio kwenye ndoa, na hii inaelezwa kuwa watu wakioana huongeza kuhusiana baina yao na maisha ya jamii.
Utafit huu ambao ulihusisha watu 800,000 kutoka Ulaya, Amerika ya Kaskazini na Kusini pamoja na Asia umeonesha kwamba watu ambao hawajawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi wako kwenye hatari ya ugonjwa huu kwa 42% zaidi ya walio kwenye ndoa.
Imebainishwa pia kuwa kwa wajane kwao hatari huongezeka kwa 20% ukilinganisha na walio kwenye ndoa hatahivyo haikuelezwa bayana kuhusu wanandoa ambao wametengana. Wataalamu wameeleza kuwa kwa ujumla wanandoa huwa na uwezo wa kuishi maisha ya afya zaidi kuliko wasio kwenye ndoa.
Ulipitwa na hii? HARUSI YA JOTI KANISANI: TABASAMU NA KIDUKU KAMA KAWAIDA