Baada ya ripoti ya CAG kutangazwa, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa nchini kuwasilisha hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2014/15 ndani ya siku 90 kabla havijachukuliwa hatua za kisheria.
Pia amevitaka vyama hivyo kuheshimu sheria za mashirika ya umma ambazo ni Sheria ya Ukaguzi wa Fedha za Umma, Sheria ya Fedha za Umma na Sheria ya Vyama vya Siasa
‘Tulishavikumbusha vyama vya siasa kuwasilisha bajeti zao, baada ya kupata taarifa ya CAG hatua inayofuata ni kuangalia taarifa hiyo na kuchukua hatua‘ –Jaji Francis Mutungi
‘Kama kutakuwa na sintofahamu katika mahesabu ya vyama vinavyopata ruzuku hatua ni pamoja na kukata kiwango kinachodaiwa, lakini tumewaambia kwenye barua kuwa wana miezi mitatu ya kukamilisha suala hili‘ –Jaji Francis Mutungi
TANZANIA INA UPUNGUFU WA SUKARI, WAZIRI MKUU IMEBIDI AONGEE BUNGENI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE